Surah Ash-Sharh in Swahili

    الشرح

    Surah Ash-Sharh in Swahili

    Read Surah Ash-Sharh in Swahili (الشرح) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 94 of the Holy Quran, 8 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

    Hatukukunjulia kifua chako? [1]

    [1] Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.

    2

    وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

    Na tukakuondolea mzigo wako! [2]

    [2] Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,

    3

    ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

    Ulio vunja mgongo wako? [3]

    [3] Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.

    4

    وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

    Na tukakunyanyulia utajo wako? [4]

    [4] Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.

    5

    فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

    Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi! [5]

    [5] Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.

    6

    إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرٗا

    Hakika pamoja na uzito upo wepesi. [6]

    [6] Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile.

    7

    فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ

    Na ukipata faragha, fanya juhudi. [7]

    [7] Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo.

    8

    وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب

    Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. [8]

    [8] Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.

    Ash-Sharh

    Play