Surah Ad-Duhaa in Swahili

    الضحى

    Surah Ad-Duhaa in Swahili

    Read Surah Ad-Duhaa in Swahili (الضحى) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 93 of the Holy Quran, 11 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    وَٱلضُّحَىٰ

    Naapa kwa mchana! [1]

    [1] Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi!

    2

    وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ

    Na kwa usiku unapo tanda! [2]

    [2] Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!

    3

    مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ

    Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. [3]

    [3] Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.

    4

    وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ

    Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. [4]

    [4] Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake.

    5

    وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ

    Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. [5]

    [5] Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.

    6

    أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ

    Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? [6]

    [6] Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?

    7

    وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ

    Na akakukuta umepotea akakuongoa? [7]

    [7] Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?

    8

    وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ

    Akakukuta mhitaji akakutosheleza? [8]

    [8] Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki?

    9

    فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ

    Basi yatima usimwonee! [9]

    [9] Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili,

    10

    وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ

    Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! [10]

    [10] Na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu,

    11

    وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ

    Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. [11]

    [11] Na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.

    Ad-Duhaa

    Play