Surah At-Tin in Swahili

    التين

    Surah At-Tin in Swahili

    Read Surah At-Tin in Swahili (التين) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 95 of the Holy Quran, 8 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ

    Naapa kwa tini na zaituni! [1]

    [1] Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.

    2

    وَطُورِ سِينِينَ

    Na kwa Mlima wa Sinai! [2]

    [2] Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.

    3

    وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ

    Na kwa mji huu wenye amani! [3]

    [3] Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.

    4

    لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِيٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٖ

    Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. [4]

    [4] Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.

    5

    ثُمَّ رَدَدۡنَٰهُ أَسۡفَلَ سَٰفِلِينَ

    Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! [5]

    [5] Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.

    6

    إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٖ

    Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. [6]

    [6] Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.

    7

    فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعۡدُ بِٱلدِّينِ

    Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? [7]

    [7] Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?

    8

    أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَٰكِمِينَ

    Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? [8]

    [8] Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?

    At-Tin

    Play