وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ
Ole wake kila safihi, msengenyaji! [1]
[1] Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.
الهمزة
Read Surah Al-Humazah in Swahili (الهمزة) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 104 of the Holy Quran, 9 verses — free online.
Quran in Swahili · all 114 Surahs
وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ
Ole wake kila safihi, msengenyaji! [1]
[1] Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.
ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ
Aliye kusanya mali na kuyahisabu. [2]
[2] Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.
يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ
Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! [3]
[3] Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?
كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ
Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. [4]
[4] Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ
Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? [5]
[5] Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?
نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ
Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. [6]
[6] Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!
ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ
Ambao unapanda nyoyoni. [7]
[7] Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.
إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ
Hakika huo utafungiwa nao [8]
[8] Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani
فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ
Kwenye nguzo zilio nyooshwa. [9]
[9] Kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.
Al-Humazah
Play