وَٱلۡعَصۡرِ
Naapa kwa Zama! [1]
[1] Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.
العصر
Read Surah Al-Asr in Swahili (العصر) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 103 of the Holy Quran, 3 verses — free online.
Quran in Swahili · all 114 Surahs
وَٱلۡعَصۡرِ
Naapa kwa Zama! [1]
[1] Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.
إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَفِي خُسۡرٍ
Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, [2]
[2] Hakika kila binaadamu bila ya shaka yumo katika namna fulani au fulani ya kukhasiri, kwa mujibu wa anavyo ghilibiwa na pumbao na matamanio.
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡحَقِّ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ
Ila wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri. [3]
[3] Isipo kuwa wale walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema, na wakadumu juu ya ut'iifu, na wakasemezana na kuusiana kwa kushikamana na Haki, kwa itikadi, na maneno, na vitendo. Na wakausiana wasubiri na wavumilie mashaka yanayo wapata wenye kushikamana na Dini. Basi hao ndio wenye kusalimika na hiyo khasara, wenye kufanikiwa duniani na Akhera.
Al-Asr
Play