Surah At-Takathur in Swahili

    التكاثر

    Surah At-Takathur in Swahili

    Read Surah At-Takathur in Swahili (التكاثر) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 102 of the Holy Quran, 8 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

    Kumekushughulisheni kutafuta wingi, [1]

    [1] Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!

    2

    حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

    Mpaka mje makaburini! [2]

    [2] Mpaka yakusibuni mauti!

    3

    كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

    Sivyo hivyo! Mtakuja jua! [3]

    [3] Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.

    4

    ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

    Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! [4]

    [4] Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!

    5

    كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ

    Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, [5]

    [5] Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.

    6

    لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ

    Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! [6]

    [6] Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.

    7

    ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ

    Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. [7]

    [7] Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.

    8

    ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ

    Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema. [8]

    [8] Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.

    At-Takathur

    Play