Surah Az-Zalzalah in Swahili

    الزلزلة

    Surah Az-Zalzalah in Swahili

    Read Surah Az-Zalzalah in Swahili (الزلزلة) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 99 of the Holy Quran, 8 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

    Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! [1]

    [1] Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!

    2

    وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

    Na itakapo toa ardhi mizigo yake! [2]

    [2] Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!

    3

    وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

    Na mtu akasema: Ina nini? [3]

    [3] Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?

    4

    يَوۡمَئِذٖ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

    Siku hiyo itahadithia khabari zake. [4]

    [4] Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,

    5

    بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

    Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! [5]

    [5] Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.

    6

    يَوۡمَئِذٖ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتٗا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ

    Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! [6]

    [6] Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.

    7

    فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرٗا يَرَهُۥ

    Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! [7]

    [7] Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.

    8

    وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ شَرّٗا يَرَهُۥ

    Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! [8]

    [8] Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.

    Az-Zalzalah

    Play