Surah Al-Qadr in Swahili

    القدر

    Surah Al-Qadr in Swahili

    Read Surah Al-Qadr in Swahili (القدر) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 97 of the Holy Quran, 5 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ

    Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. [1]

    [1] Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.

    2

    وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ

    Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? [2]

    [2] Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?

    3

    لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ

    Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. [3]

    [3] Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.

    4

    تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

    Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. [4]

    [4] Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.

    5

    سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ

    Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. [5]

    [5] Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

    Al-Qadr

    Play