Surah Al-Ala in Swahili

    الأعلى

    Surah Al-Ala in Swahili

    Read Surah Al-Ala in Swahili (الأعلى) with Arabic text, Swahili translation, and audio recitation. Chapter 87 of the Holy Quran, 19 verses — free online.

    Quran in Swahili · all 114 Surahs

    1

    سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى

    Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa! [1]

    [1] Litakase jina la Mola wako Mlezi lilio tukufu na kila kitu kisicho kuwa kinaelekeana nalo.

    2

    ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ

    Aliye umba, na akaweka sawa! [2]

    [2] Aliye umba kila kitu, na akajaalia uumbaji wote sawa sawa katika hukumu na kupangana.

    3

    وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ

    Na ambaye amekadiria na akaongoa,. [3]

    [3] Na akakadiria kwa kila kitu kwa mujibu wa maslaha yake, na akakiongoza.

    4

    وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ

    Na aliye otesha malisho! [4]

    [4] Na ambaye akatoa kwenye ardhi mimea namna mbali mbali ya kuwalisha wanyama.

    5

    فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ

    Kisha akayafanya makavu, meusi. [5]

    [5] Na akaifanya mimea hiyo baada ya kuwa kijani imestawi, ikakauka na imekuwa myeusi!

    6

    سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ

    Tutakusomesha wala hutasahau! [6]

    [6] Ewe Muhammad! Sisi tutakujaalia uwe ni mwenye kuisoma Qur'ani kwa ufunuo kutoka kwetu, na wala hutosahau utacho kihifadhi.

    7

    إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ

    Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. [7]

    [7] Isipo kuwa anacho taka Mwenyezi Mungu ukisahau, kwani hakika Yeye Mtukufu anayajua wanayo yadhihirisha waja wake na wanayo yaficha, ikiwa maneno au vitendo.

    8

    وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ

    Na tutakusahilishia yawe mepesi. [8]

    [8] Na tutakuwezesha kupita njia ya kufikilia kwa wepesi mambo yako yote.

    9

    فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ

    Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. [9]

    [9] Basi wakumbushe watu ikiwa kukumbusha kutaleta manufaa, kwani inavyo faa ndio kuwanafiisha.

    10

    سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ

    Atakumbuka mwenye kuogopa. [10]

    [10] Watanafiika kwa ukumbusho wako wanao mwogopa Mwenyezi Mungu.

    11

    وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى

    Na atajitenga mbali nayo mpotovu, [11]

    [11] Na atajitenga na ukumbusho mpotovu anaye shikilia kufanya inda na ukafiri.

    12

    ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ

    Ambaye atauingia Moto mkubwa. [12]

    [12] Ambaye ataingia kwenye Moto mkubwa ulio andaliwa kuwa ndio malipo yake.

    13

    ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ

    Tena humo hatakufa wala hawi hai. [13]

    [13] Tena hatokufa huko Motoni akapumzika kwa kifo, wala hawi hai kwa uhai wa kustarehe nao.

    14

    قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ

    Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. [14]

    [14] Hakika amefuzu mwenye kujisafisha na ukafiri na maasi.

    15

    وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ

    Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali. [15]

    [15] Na akalikumbuka jina la Muumba wake kwa moyo wake na ulimi wake, na akaswali kwa unyenyekevu kama itakikanavyo.

    16

    بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

    Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! [16]

    [16] Bali nyinyi hamfanyi hayo yanayo pelekea kufanikiwa, lakini katika hima zenu mnatanguliza maisha ya duniani kuliko ya Akhera.

    17

    وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ

    Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. [17]

    [17] Na Akhera ni bora kuliko dunia, kwa usafi wa neema zake, na ni yenye kubaki na kudumu zaidi.

    18

    إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ

    Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, [18]

    [18] Hakika haya yote yaliyo tajwa katika Sura hii bila ya shaka yamethibitishwa katika Vitabu vya zamani,

    19

    صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ

    Vitabu vya Ibrahimu na Musa. [19]

    [19] Vitabu vya Ibrahimu na Musa; kwani haya yamewafikiana na mafunzo ya dini zote na yamesajiliwa katika Vitabu vya mbinguni.

    Al-Ala

    Play